RC KATAVI ATOA MIEZI MITATU KWA MANISPAA YA MPANDA KUBORESHA MASOKO


1 
Mkuu wa Mkoa wa  Katavi Mhe.Amosi Makalla amebaini pamoja na wafanyabiashara kulipa ushuru baadhi ya MASOKO makubwa hayana Maji , Umeme, Mageti na vyoo
2
Hata hivyo amewataka watendaji wa masoko kutoza ushuru kwa mujibu wa sheria na kuacha kuwatoza tozo ambazo hazipo kisheria
Mkuu wa mkoa wa Katavi Leo ametembelea soko kuu la Mpanda na kufanya mkutano wa hadhara wa KUSIKILIZA kero za wafanyabiashara wa soko Kuu, Mpanda Hotel, Buzogwe, Azimio na Stendi Kuu
3
Baada ya kusikiliza kero amebaini masoko mengi hayana huduma ya Maji, umeme , vyoo na mageti kwa ajili ya usalama
4
Aidha amebaini baadhi ya wafanyabiashara kutozwa ushuru kwa kutofuata sheria zilizowekwa Kutokana na Hali hiyo ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa manispaa kuboresha huduma za masoko

No comments

Powered by Blogger.