SERIKALI KUWAFUTA MACHOZI WADAU WA ZAO LA EMBE
Serikali imeahidi kuwasaidia
Chama cha Wakulima wa Embe Nchini Amagro kupata huduma ya nishati ya Umeme
katika vituo vyake vya ukusanyaji na usindikaji wa bidhaa za embe Wilayani Mkuranga.
Hayo yamesemwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Ludovick Nduhiye
ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa
Wadau wa Zao la Embe ambao umefanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K.
Nyerere,barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
Bw.Nduhiye amesema kuwa atahakisha
anawasiliana na Taasisi zinazohusika na maswala ya nishati ya umeme ili waweze
kupeleka nishati hiyo katika kituo hicho cha usindikaji wa embe Wilayani Mkuranga
ambacho kimeombewa umeme kwa miaka minne mpaka hivi sasa hakijapata huduma hiyo
kutokana na kuwa mbali na vyanzo vya umeme.
Wakati wa Mkutano huo, Wadau
wa Embe katika mnyororo wa thamani waliomba Serikari kuwasaidia miundombinu ya
usafirishaji na uhufadhi wa embe, ambapo Naibu Katibu Mkuu ameahidi kuwasiliana
na Wizara ya Kilimo ili waweze kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Mkutano huo umeratibiwa kwa
ushirikiano wa Umoja wa Wakulima wa Zao la Embe (AMAGRO) pamoja na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
No comments