RC KATAVI ATOA MIEZI MITATU KWA MANISPAA YA MPANDA KUBORESHA MASOKO
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Amosi Makalla amebaini pamoja na wafanyabiashara kulipa ushuru baadhi ya MASOKO makubwa hayana Maji , Umeme, Mageti na vyoo
Hata hivyo amewataka watendaji wa masoko kutoza ushuru kwa mujibu wa sheria na kuacha kuwatoza tozo ambazo hazipo kisheria
Mkuu wa mkoa wa Katavi Leo ametembelea soko kuu la Mpanda na kufanya mkutano wa hadhara wa KUSIKILIZA kero za wafanyabiashara wa soko Kuu, Mpanda Hotel, Buzogwe, Azimio na Stendi Kuu
Baada ya kusikiliza kero amebaini masoko mengi hayana huduma ya Maji, umeme , vyoo na mageti kwa ajili ya usalama
Aidha amebaini baadhi ya wafanyabiashara kutozwa ushuru kwa kutofuata sheria zilizowekwa Kutokana na Hali hiyo ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa manispaa kuboresha huduma za masoko
No comments